BAADA YA KIPIGO, HASSAN KESSY ASEMA SIMBA WALIBEBWA NA MWAMUZI



Baada ya kupigwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Taifa jana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, beki wa kulia wa Nkana Red Devils, Hassa Kessy, amesema Mwamuzi alikuwa amelalia upande wa wapinzani wao Simba.

Kessy ambaye aliwahi kucheza soka Simba na Yanga, amefunguka kuwa Mwamuzi huyo hakuzimudu dakika 90 kwa kuchezesha vizuri jambo ambalo lilipelekea Simba wakapata matokeo.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, Kessy alieleza Simba waliwamudu vizuri lakini mwisho wa siku matokeo ya mchezo yalijitokeza wakipoteza.

Aidha, alisema kuwa walipata nafasi nyingi za kufunga na zikashindwa kuleta mafanikio badala yake wakashindwa kuzitumia vizuri.

Nkana sasa imeshuka mpaka kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo wataanza rasmi maandalizi ya kujiandaa na mechi za mashindano hayo mapema baada ya kurejea kwao Zambia.

Comments