Hatimae Mbwana Samatta amerudishiwa Golden Bull tena


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta usiku wa December 17 2018 alikuwa sehemu ya kikosi cha KRC Genk kilichocheza dhidi ya KV Oostende wakiwa nyumbani katika mchezo wao wa 16 wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2018/2019.
Samatta ambaye alikuwa sehemu ya mchezo huo alifanikiwa kuisaidia KRC Genk kupata ushindi wa magoli 2-0, goli la kwanza likifungwa na Ruslan Malinovsky dakika ya 34 na Mbwana Samatta akafunga goli la mwisho dakika ya 74, hivyo ushindi huo ukaifanya Genk kuendelea kuongoza kwa kuwa na point 42.
Hata hivyo Samatta katika game hiyo goli lake limemfanya kuwa kinara wa magoli ndani ya club ya Genk na Ligi Kuu kwa ujumla akiwa na jumla ya magoli 12, akifuatiwa na Ivani Santini wa Anderletch kwa kuwa na magoli 11, baada ya kuongoza kwa magoli Samatta anarudishiwa Golden Bull katika jezi yake mgongoni kama ishara ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi.

Golden Bull huwa inawekwa kama nyuma ya jezi ya mchezaji mwenye magoli mengi KRC Genk ila akipitwa na mtu inaondolewa.

Comments