Mo Rashid matumaini kibao KMC

Mohamed Rashid anaamini kujiunga na KMC kutarejesha makali yake na baadaye kurudi Simba kupigania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
“Namshukuru mwalimu wangu Patrick Aussems kwa kuniruhusu nichague timu ambayo itanisaidia kurudi kwenye kiwango nilichokuwanacho tangu Tanzania Prisons na ninaamini kuja hapa (KMC) kiwango changu kitarudi kama mwanzo.”
“Kikubwa ni kujituma na kujiamini, nina imani nitarudi kama mwanzo na watu wataamini mimi ni yuleyule niliyetoka Prisons kwenda Simba na baadaye kutolewa kwa mkopo.”
“Kocha wa KMC alikuwa ananifatilia tangu nikiwa Tanzania Prisons na amenipigania hadi nimekuja kwenye timu yake anaimani nina kitu ambacho nitaisaidia timu nikishirikiana na wenzangu.”
Mohamed Rashid amejiunga na KMC kwa mkopo wa miezi sita akitokea Simba ambako alisajiliwa akitokea Tanzania Prisons.

Comments
Post a Comment