Shaibu asisahau kufua soksi za Canavaro

Abdallah Hajji Shaibu ‘ninja’ ni moja ya mabeki wanaopatikana katika kikosi cha wanajangwani dar es salaam young Africans,kijana huyu alisajiliwa akitokea jang’ombe ya Zanzibar baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya mapinduzi cup kitendo kilichopelekea aliyeekua kocha wa yanga kwa wakati huo Charles Boniphace Mkwasa kumsajili na kumpa mkataba wa miaka miwili.
Abdallah shaibu ni mchezaji anaefananishwa na nahodha wa zamani wa yanga Nadir haroub maarufu kwa jina la Canavarro kutokana na aina ya uchezaji wake pamoja na kujituma kwake anapokua uwanjani, sanjari na hilo Ninja anavalia jezi namba 23 ilokua ikitumia na canavarro wakati akiitumikia timu ya wananchi dar young Africans hii ni baada ya Nadir kukataa jezi ake kustafishwa wakati wa mechi ya heshima maalumu dhidi ya mawenzi market ya morogoro ilokua mechi ya kumuaga beki huyo wa yanga aloitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka kumi na kuipatia mafanikio makubwa.
Baada ya usajiri huo ninja amekua akitumika kwenye kikosi cha wanajangwani katika sehemu tofauti tofauti kama beki na wakati mwingine kama kiungo mkabaji kutokana na aina ya mfumo na mahitaji ya mwalimu na amekua akifanya vizuri, mwanzo shaibu alikua akionekana kama mchezaji mwenye mwenye mapungufu mengi hasa palwe anapokua anamkaba mpinzani kwani alikua akisababisha faulo nyingi zisizo na umsingi. Lakini kadri ya mda unavoenda shaibu ameonesha samani ya jezi aliyorithi kwani mwezi ulopita alifanya vizuri na kufikia kuingia kwenye tatu bora ya mwezi November akishindana na washambuliaji makambo na dilunga na makambo kuwashinda na kua mchezaji bora wa mwezi November.
Mechi ilopita yanga walichweza na biashara fc ya mara na mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Biashara fc walikua mbele kwa goli 1 lakini kipindi cha pili ‘NINJA’ Alisawazisha na baadae makambo akaweka kambani na kuwawezesha yanga kujiongezea pointi tatu muhimu, huku Shaibu akionesha kiwango cha hali ya juu na ni wakati ambao anatakiwa kujituma zaidi na zaidi ili aweze kufiti kwenye viatu na soksi alokua anazivaa kaka ake Mzanzibar Haroub Canavarro na kuweza kucheza kwa mda mrefu. Cha msingi ambacho anatakiwa kufanya ni kuueshimu mwili ake, kufanya mazoezi, kula vyakula vyenye kujenga mwili na kumsikiliza kocha kipi anataka kwake na aachane na maisha ya anasa atafanikiwa na kuwa mchezaji mkubwa hapa nchini na Africa.

Comments