Simba wamefungua milango lakini wakumbuke madirisha yapo wazi


WAwakilishi wa Tanzania kimataifa na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba sports club wapo kwenye maandalizi makali kuelekea mechi ya kimataifa dhidi ya Nkana Red deviels kutoka nchini Zambia, Simba imetoka kuwatoa mbambane swallows ya Zimbabwe kwa jumla ya magoli 8 dhidi ya 1 la mbambane katika mechi zote mbili.
Simba ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ligi kuu Tanzania bara ikiwa na jumla ya pointi 27 ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 ikipoteza 1 sare 3 na kushinda mechi 8 ikiwa nyuma ya vinara wa ligi
Yanga wenye pointi 41 wakifatiwa na azam wenye pointi 40. Pamoja na samba kua nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi mpaka sasa samba iko nyuma kwa idadi ya mechi dhidi ya vinara yanga kwa mechi tatu.
Simba inakaa takribani wiki moja na siku mbili kabla ya kuwavaa wapinzani wao kimataifa nkana Fc ambapo katika wakati huo ligi itakua inaendelea na kupelekea kuongeza idadi ya viporo ambayo inapunguza na kuharibu mvuto wa ligi hasa kuelekea kumpata bingwa.
Simba inaelekea kua wanafurahia huu mda mrefu wanaopewa na bodi ya ligi kwenye maandalizi yao ya mechi za kimataifa lakini changamoto kubwa inakuja kwenye ratiba hasa mwezi huu mwishoni pale mapinduzi cup itapokua imeeanza huko Zanzibar.
Kutokana na matokeo ambayo yanga na azam wanaendelea kuyapata kwenye ligi kuu Tanzania bara yanazidi kutengeneza presha kubwa dhidi ya simba ambayo sasa ipo imewekeza muda mwingi kwenye michezo ya kimataifa huku wakisahau kuwa ili washiriki mara nyingi iwezekanavyo kwenye mashindano haya ya kimataifa inabidi pia wawe na mfululizo wa matokeo mazuri kwenye ligi ya ndani pasipo kuathiri ratiba ya ligi ama kimataifa.
Kwani itafikia kipindi ambacho ratiba itakua so rafiki kwao na wachezaji kukujmbwa na uchovu ambao unaweza pelekea timu kutofanya vizuri.
Mpaka sasa sioni sababu ya bodi ya ligi pamoja na TFF Kuzipa mda mrefu simba na mtibwa sugar kwa kivuri cha mechi za kimataifa wakati ratiba za kimataifa ya FIFA na CAF inaeleweka na hutolewa kabla ya ligi zote kuanza hivo hizi sababu za timu moja kua na viporo limekaa kisiasa na linaweza pelekea upangaji wa matokeo unaoweza kuchafua sifa na mwelekeo wa soka la nchi yetu.
Ni mda mwafaka ambapo samba, TFF na bodi ya ligi kuliangalia hili katika jicho sahihi kwani linaweza kuiathiri samba au ligi kwa ujumla na samba kutumia mda wao mwingi kufikilia juu ya mechi za kimataifa pasipo kuamgalia ligi kuu Tanzania bara ni sawa na kufunga mlango huku dirisha ukiwa umeacha wazi .

Comments