SINGIDA UNITED YAPANGA KUMPELEKA ULAYA MCHEZAJI WA YANGA



Uongozi wa Singida United umesema kuwa mpango wa kuwaachia wachezaji wake wawili John Tiber na Kenny Ally kujiunga na Yanga bado ni mapema kuuzungumzia kwa kuwa wana mipango nao ndani ya kikosi cha kuwafanya wawe ni wachezaji wa kimataifa.

Keny na Tiber wamekuwa wakielezwa kuhitajiwa  na Yanga katika usajili wa dirisha dogo ambao unafungwa Desemba 15 baada ya kufunguliwa Novemba 15 mwaka huu.


Ofisa habari wa timu ya Singida United, Cales Katemana amesema kuwa kwa sasa hawana mpango wa kuwatoa wachezaji wake kwenye timu za ndani mipango yao ni kuweza kuwapeleka wachezaji hao nje ya nchi kucheza soka.

"Tiber anaweza kuondoka mwezi wa kwanza ama januari kuelekea kuitumika timu ya Czech ya barani ulaya kwa makubaliano yenye faida kwa timu pamoja na mchezaji mwenyewe ili aweze kuwa bora zaidi ya alipo sasa.


"Kenny bado tupo naye ndani ya kikosi kwa kuwa bado ana mkataba wa miezi sita ndani ya timu hivyo suala la yeye kuondoka kwenye timu bado kwa sasa ataendelea kuitumikia timu yetu hawezi kwenda Yanga," alisema.

Comments