TFF wasipowaelewa Simba hata Mtibwa hawatawaelewa

Simba na Mtibwa zimefanya vibaya. Nadhani kila mtu amemuona Chama na Mkude. Simba walionekana wakwaida sana. Yule Chama aliyewasumbua Mbabane Swallows jana hakuonekana katika ubora wake. Hivi tumejiuliza kwanini Chama alishindwa kung’ara? Ni kwa sababu ya kikosi kizima kushindwa kucheza kwa uweledi.
Kilichosababisha haya ni kutokana na ubovu wa ligi. Chama ameonekana bora kwe ye ligi mbovu. Ligi ambayo timu kama Ndanda zinakwama kukosa usafiri. Leo hii Stand United haijui Kitenge yupo wapi.
Kila timu inalalamika njaa. Inategemea ushindani gani hapa wa kwenda kucheza na Nkana waliotoka kumfumua Zesco bao tatu ugenini? Ni Nkana hawa hawa ambao katika mechi 22 hawajafungwa mchezo hata mmoja.

Chama na Mkude walishindwa kufurukuta mbele ya Chisala , lakini sio kwa sababu Chama na Mkude hawana uwezo, hapana, ni kwa sababu Simba imezoea vya kunyonga sio vya kuchinja. Simba ilishindwa kulinda ubora wa Chama. Hakuna mchezaji anayefurukuta mbele ya wachezaji 11 pekee yake. Unahitaji kulindwa na wale wanaokuzunguka. Tazama Lionel Messi aliyecheza Wembley dhidi ya United 2012 akiwa amezungukwa na Xavi na Iniesta na Villa, Halafu jaribu kumtazama Messi aliyecheza na Roma aliyezungukwa na Ivan Rakitic? Hebu kumbuka kiwango cha Pogba aliyecheza mbele ya Pirlo, Vidal na Marchisio? Na huyu Pogba wa Man United.
Simba imeshindwa kumlinda Chama, kwa sababu ligi nayo imesihindwa kuilinda Simba. Ligi yetu ni dhaifu mno. Simba ina wachezaji wazuri sana na wenye uwezo mkubwa tutizo ni changamoto wanazokutana nazo ni nyepesi mno. Ukinfunga Ruvu Shooting 5 ni jambo la kusikitisha yaani sio la kujivunia. Yaani inapaswa kila unayekutana nae awe mkorofi, ligi iwe ya kutibuana tibuana.
Kwa mfano ndugu zetu hawa Mtibwa kwenda Shirikisho ni kama ngekewa kwao. Kimaandalizi na kisaikolojia hawakuwa wamejiandaa katika hili. Wanakwenda kucheza na KICC ambayo katika mechi zake mbili za klabi bingwa msimu uliopita walifanikiwa kuwafunga miamba ya Afrika jumla ya mabao 5 katika mechi 2
Esperance 4-3 KICC
Al Ahly 3-2 KICC
Al Ahly 3-2 KICC

Hata Simba yenye kuweza kufunga idadi ya magoli hao kwa miamba hao ni mtihani mgumu sana. Mfumo tuliojiwekea wa Bingwa wa FA kwenda kucheza Shirikisho ni wa ajabu sana. Mtibwa hawajafanya uwekezaji wowote ule walitaka kwenda wapi? Kufanya nini? Wakati usajili unaanza kwanini hawakuomba msaada kwa kupata angalau wachezaji wenye uzoefu kwa mkopo? Kwanini hawakuomba msaada kutoka TFF iwapatie wepesi wa kupata wachezaji? Zambia ina timu 4 zinazokwenda kimataifa kwa sababu ya viwango vya Zesco na Nkana wanakuwa wanafanya vyema michuano ya kimataifa. Je sisi hatuoni umuhimu wa kuvisaidia vilabu vyetu kwenda mbali ilikutoa fursa na sisi vilabu vinne vishiriki?

Unapocheza michuano ya kimataifa kule hakuna Lipuli hakuna Mwadui kule kuna miamba ya ligi mbalimbali. Kwa uwezo ule wa mtibwa wamekwenda kupigana vita ambayo haikuwahusu hasa kwa maandalizi yao yale.
Shida nyingine kubwa ipo kwa TFF ambao wanatumia nguvu nyingi kwenye mambo ambayo sio ya msingi na hayana tija kwa taifa. Badala watengeneze ligi ngumu wao wanatengeneza ligi nyepesi. Unapoweka timu 20 kwenye ligi ambayo umasikini umewatala ni sawa na kuweka Swala wengi kwenye kundi la Simba na Tembo mkiamini wingi wao utawafanya wawe na makucha.
Tunachekesha. TFF walijua wazi vilabu vingi vinategemea fedha za Azam na Mdhamini, mdhamini ameondoka lakini wao wanaongeza timu 20. Kila kukicha mara yule kakosa nauli, mara Beno hajulikani alipo, mara tumekosa hela ya maji, mara fulani amegoma kuingilia geti kubwa na TFF wanaona na wanajifanya hawaoni.

Hivi inakuwaje umasikini na ushirikina unatutafuna kila kukicha na viongozi wapo wanashindania mafaili ya kesi za Wambura? Yaani sakata la Wambura limekuwa kipaumbele kule hata ligi yenyewe..
Hakukuwa na haja ya timu 20 ni heri ziwepo timu 10 ngumu ambapo bingwa anabeba ubingwa kwa kucheza game 19 ngumu kuliko kucheza mechi 38 halafu mechi 6 pekee ndo ngumu 32 zilizobaki zikawa nyepesi. Kila kambi ya timu za ligi zinalia njaa.
Punguzeni timu ziwe 10 au 12, ongezeeni kombe la 3 kisha rudisheni kombe la Muungano. Ni heri upambane na maadui 4 wemye nguvu kuliko maadui 100 wabovu. 
Tumekuwa na desturi ya kuwasifia wachezaji wetu pindi wanapocheza na timu dhaifu mnoo. Tunawabebea hadi mabango. Yamkini hawana uwezo ni kwa sababu tu wanacheza na timu dhaifu.

Tumekuwa na desturi ya kuwasifia wachezaji wetu pindi wanapocheza na timu dhaifu mnoo. Tunawabebea hadi mabango. Yamkini hawana uwezo ni kwa sababu tu wanacheza na timu dhaifu.
Mwisho:
Shida ya Simba sio Kikosi chao ila ubovu wa ligi, shida ya Mtibwa sio ubovu wa ligi, ila mipango ya kupata muwakilishi wa kimataifa ni mibovu na mipango ya kumsaidia muwakilishi wa kimataifa pia mbovu.
Mashabiki wa Simba wanalalamika basi walilopanda liliwekewa mambo ya ajabu, na ndio basi lile lile ambalo Simba walipaswa kupanda, Je Simba kwanini masuala ya usafiri na malazi wasiwe wanaratibu wenyewe kupitia ubalozi wao? Tatizo.

Comments
Post a Comment