WABAYA WA SIMBA NA YANGA HAWA HAPA, KUVAANA JANUARI
MASHINDANO ya Mapinduzi Cup yanatarajiwa kuanza Januari Mosi na kumalizika Januari 13 yakihusisha timu 9 ambazo zitagombania ubingwa ulio mikononi mwa Azam FC.
Mabingwa watetezi Azam FC, watashuka uwanjani Januari 2 kuvaana na Jamhuri, huku Yanga watashuka uwanjani Januari 03 kuvaana na KVS, Simba wao Januari 4 watamenyana na Chipukizi.
Kombe hilo litafanyika Zanzibar lina makundi mawili ambayo yana timu 4 isipokuwa kundi B lina timu tano ambazo zinashiriki.
Kundi A lina timu kama Chipukizi, Mlandenge, KMKM na Simba huku B likiwa na timu 5 ambazo ni KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.
Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo imesema kuwa Zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka milioni 10 mpaka milioni 15 ikiwa ni pamoja na medali za dhahabu pamoja na kombe.
Mashindano hayo yatatumia uwanja wa Amaan kwa mechi zote mpaka nusu Fainali na Uwanja wa Gombani kwa mechi ya Fainali.
Comments
Post a Comment