WACHEZAJI AMBAO ZAHERA ALIPENDEKEZA WAMWAGE WINO DIRISHA DOGO

Baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa Disemba 15, imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga alipendekeza baadhi ya wachezaji kusajiliwa lakini mabosi wake wakafanikiwa kumnyaka Haruna Moshi pekee.
Kitendo hicho kimeonesha kumkera Zahera na kuwaambia endapo Yanga itaukosa ubingwa basi asilaumiwe.
Kocha huyo ambaye amekuwa hana unafiki tangu ajiunge na Yanga, ameeleza kuwa kuna usajili umefanyika ambao haukuwa pendekezo lake.
Moja ya usajili huo ni ule wa kipa Ibrahim Hamid ambao hakuupendekeza lakini mabosi wake wakaamua kumsajili.
Wachezaji ambao imeelezwa Zahera aliwapendekeza ni hawa hapa:-
1. Farouk Shikhalo (Bandari)
2. Haruna Moshi Baban (African Lyon)
3. Charles Ilanfia (Mwadui FC)
4. Umar Kasumba (Sofapaka)

Comments
Post a Comment