azam fc kuanza na hawa leo kutetea kombe la mapinduzi



KOCHA msaidizi wa kikosi cha Azam FC, Juma Mwambusi amesema wapo tayari kwa mchezo wao wa leo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri utakaochezwa leo Uwanja wa Amaan saa 2 Usiku.

Mwambusi amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano kutokana na kujiaanda vizuri wana imani ya kupata matokeo yatakayowasaidia kufanikiwa kutetea ubingwa wao.

"Tupo sawa wachezaji tayari tumewapa mbinu mpya zitakazosaidia kupata ushindi kwenye mchezo wetu, ni mabingwa watetezi inatupasa tucheze kibingwa kupata matokeo mazuri," alisema.

Mchezo mwingine ambao utaanza leo mapema ni ule dhidi ya Chipukizi na Mlandege FC utakaochezwa saa 10:00 jioni na mechi zote zitaonyeshwa Azam TV.

Comments