BAADA YA KILUVYA UNITED KUNUNULIWA TIMU NYENGINE

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amethibitisha kuwa Dodoma FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza rasmi itachukuliwa kutoka mikononi mwa wananchi na itasimamiwa na Halmashauri ya Jiji hilo kuanzia mwezi wa pili mwaka huu.
Kunambi amesema timu hiyo pia itabadilishwa jina ikiwa ni miongoni mwa hatua za kuboresha sekta ya michezo jijini humo, huku akieleza Imani yake kuwa Dodoma FC itapanda daraja na kuwa tishio kwa vigogo wa soka nchini Simba na Yanga.
Amesema halmashauri hiyo pia imeanza mkakati wa kujenga viwanja vidogovidogo vya michezo katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo licha ya serikali kutenga eneo maalumu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Dodoma utakaojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Morocco.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma sasa imejidhatiti kurejesha heshima ya jiji hilo katika nyanja za michezo iliyotoweka miaka kadhaa iliyopita baada ya timu zake zilizokuwa zikishiriki ligi kuu wakati huo zikiwemo, Kurugenzi, Waziri Mkuu, Polisi Dodoma, na Mji Mpwapwa kushuka daraja.

Comments
Post a Comment