hawa wapinzani wa simba Sj Saoura ni tabu tupu



Unaambiwa wapinzani wa klabu ya Simba kutoka Algeria, JS Saoura wamekuwa wakiifatilia Simba kila kona ili kuijua vizuri.

Timu hiyo ambayo ni miongoni mwa zile zilizo kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kupitia ukurasa wake wa Facebook imekuwa ikiweka picha mbalimbali za Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameposti picha ambayo Saoura wameiweka na kuielezea kuwa wanashangazwa na umati ambao wekundu hao wa Msimbazi wanajaza Uwanjani.



Comments