makambo alivyowatesa simba

Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji wa Yanga, raia wa DR Congo, Heritier Makambo, kuandika rekodi ya pekee hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimshinda mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi msimu uliopita.
Rekodi hiyo si nyingine bali ni ile ya kupachika mabao mengi katika mechi za mikoani ambazo Yanga imecheza mpaka sasa dhidi ya Mwadui FC, Kagera Sugar, Prisons, African Lyon pamoja na Mbeya City. Katika mechi hizo, Yanga imefanikiwa kushinda zote huku ikijipatia mabao 10 ya kufunga lakini pia ikifungwa manne.
Katika mechi dhidi ya Mwadui FC ilishinda 2-1, ikaichapa Kagera Sugar 2-1, ikaifunga Prisons 3-1, kisha ikaichapa 1-0 Afican Lyon na juzi Jumamosi kifanya tena hivyo dhidi ya Mbeya City kwa kuifunga mabao 2-1.
Katika mabao hayo 10 ambayo Yanga imefunga mikoani, manne kati ya hayo yamefungwa na Makambo na kufanikiwa kuandika rekodi ya pekee ambayo msimu uliopita licha ya Okwi kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 20, alishindwa kuiandika rekodi hiyo.

Comments
Post a Comment