SIMBA YAWATUMIA SALAMU CHIPUKIZI, KUANZA NA KIKOSI KAMILI LEO

SIMBA leo itakuwa kwenye mchezo wao wa kwanza wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Chipukizi ambao wana maumivu ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mlandege.
Simba wapo Zanzibar na kikosi cha kwanza huku hesabu zao kubwa ikiwa ni kutumia michuano hiyo kuandaa kikosi kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Caf ambayo Simba wanashiriki.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema wapo tayari kwa ajili ya kupambana kwenye michuano hiyo na wanawaheshimu wapinzani wao.
"Tumejipanga na tumekuja na kikosi kamili kwa ajili ya kuleta ushindani, tuna imani tutafanya vizuri kwani michuano hii ni mikubwa na ya heshima kwetu," alisema.

Comments
Post a Comment