UCHAGUZI WA YANGA WAFIKIA PATAMU MAMBO YAMEIVA

Imeelezwa kuwa Kamati ya Soka ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) inaelekea kukamilisha mchakato wa kupata majina ya mwisho ambayo yatahusika katika uchaguzi wa Yanga.
Taarifa inasema kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ally Mchungahela, ameeleza kuwa wapo katika hatua za mwisho kutangaza majina hayo.
Mchungahela amefunguka kuwa kinachoelekea kukamilishwa hivi sasa ni suala la rufani pekee ambalo linafanyiwa kazi ambalo litakamilika wiki hii.
Yanga itafanya uchaguzi wake kujaza nafasi za wagombea zilizo wazi baada ya kadhaa kuachia ngazi kwa sababu zao mbalimbali.
Uchaguzi huo ambao utafanyika Januari 9 2019, utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi TFF.

Comments
Post a Comment