WACHEZAJI WA YANGA WALIOMFUATA KAKOLANYA KWAKE ILI APATE MSAMAHA WATAJWA
Sakata la kipa namna moja wa Yanga, Beno Kakolanya na Kocha wake, Mwinyi Zahera limezidi kushika kasi kutokana na wawili hao kila mmoja kuwa na njia yake hivi sasa.
Suala hili limezidi kuteka vyombo vya habari kufuatia Zahera hivi karibuni kutangaza kutomhitaji mchezaji huyo kutokana na kugoma kucheza mechi kisa madai yake.
Kufuatia sakata hilo Zahera amewaibua wachezaji wake kuwa walienda kwake na Kakolanya ili kufanya mpango wa kufikia makubaliano ya kurejea Yanga.
Kwa mujibu wa Zahera mwenyewe, amewaja wachezaji Kelvin Yondani, Andrew Vincent na Abdallah Shaibu Ninja kuwa walimfuata Kakolanya kwao kwa ajili ya kusuluhisha suala hilo.
Mkongomani huyo amefunguka kuwa wachezaji hao waliamua kumfuata Kakolanya wakimshawishi arejee kikosini lakini amekuwa mgumu na akitia ngumu pia kuomba msamaha kwa Zahera.
Mpaka sasa bado haijajulikana kama Kakolanya ataenda kumuomba msamaha Zahera ambaye ameonekana naye kuwa mgumu hata kusikia jina lake.

Comments
Post a Comment