yanga yaangukia pua simba yaanza kibabe huku



KOCHA mkuu wa timu ya Simba Queens, Omary Mbweze amesema watapambana ili kutwaa ubingwa wa Ligi ya wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzanite ya mkoani Arusha.

Mbweze amesema wanatambua ugumu waliokutana nao msimu uliopita kutokana na kushindwa kufanya vizuri hivyo hesabu kubwa kwa sasa amezielekeza kwenye ushindi kwa kila mchezo.

"Tumejipanga sawa msimu huu kwani tuna wachezaji makini ambao wanajua kuwajibika wakiwa uwanjani, nina imani tutafanikiwa kuendelea na moto wetu msimu huu bila kuogopa wapinzani wetu," alisema.

Wakati Simba Queens wakianza vizuri, Yanga Princes ambao wamepanda daraja msimu huu na kushriki ligi ya wanawake walianza kwa  kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Sister FC ya Kigoma, Alliance Girls walishinda kwa mabao 7-1 dhidi ya Panama, Mapinduzi Queens ilifungwa mabao 6-0 dhidi ya Mlandizi Queens na Baobao Queens ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Marsh Queens.

Comments