ZAHERA ATANGAZA KUTEMA WACHEZAJI YANGA, HATAKI UTANI KABISA



Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema haoni shida kumtema mchezaji yoyote katika kikosi chake endapo akishindwa kuafikiana na matakwa yake.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, Zahera ameeleza kuwa anahitaji wachezaji ambao wanajituma katika timu na si kwenda kinyume na maagizo anayoyatoa.

Aidha, Zahera amefunguka kuwa wachezaji wake wote wanapaswa kuwajibika kwa ajili ya kuisaidia timu haswa kipindi hiki ikipitia wakati mgumu.

Mkongomani huyo amesema anapenda wachezaji wakubaliane na hali iliyopo klabuni hivi sasa kwani inapitia mpito ambao bado haijajulikana lini mambo yatakuwa sawa.

Licha ya kuelezea hayo, kikosi cha Yanga ambacho kimejazwa na vijana wengi kipo Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Kikosi hicho jana kilicheza mechi ya kwanza ya kwanza dhidi ya KVZ na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shaban Mohammed dakika ya 76 ya mchezo.

Comments