KITUO KINACHOFUATA SASA KWA SIMBA NI JS SAOURA, KESHO KAZI IPO


BAADA ya kumaliza kazi kwa mafanikio makubwa kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara kwa kikosi cha Simba huku msemo wa kituo kinachofuata ukijipatia umaarufu sasa ni zamu ya JS Saoura nchini Algeria.

Simba wanaifuata JS Saoura wakiwa na kumukumbu ya kubeba pointi tatu kwenye mchezo wao uliopita Uwanja wa Taifa kwa ushindi wa mabao 3-0 watamenyana na wapinzani wao kesho ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya Makundi.

Beki kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema wanatambua umuhimu wa mchezo na ugumu wa ushindani namna ulivyo kutokana na kila timu kupiga hesabu za pointi tatu.

"Tumekamilisha salama michezo yetu ya ligi sasa huku ambako tupo ni hatua nyingine, hakuna wepesi kutokana na kushindana na mabingwa wenzetu.

"Ni kituo chenye ushindani na kila mmoja hesabu zake ni kuibuka kidedea ila bado tunaimani tutapata matokeo sapoti ya mashabiki iwe pamoja nasi," amesema Wawa.

Comments