POGBA AHAMIA BARCELONA



MAN United ina mtihani mgumu wa kukutana na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini kiungo wao, Paul Pogba ametoa kauli inayohusu wapinzani wao hao. 

Pogba anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya wababe hao wa Hispania mwezi ujao, lakini amesema amekuwa akivutiwa kuitazama Barcelona mara nyingi.

“Barcelona ni timu ambayo mara nyingi naitazama, unaweza kujifunza kama kiungo, wanacheza soka zuri, tamaduni yao na mengine mengi yanaweza kunifunza.

“Barcelona ni moja ya timu bora duniani, wana wachezaji wengi wazuri, mechi dhidi yao naamini itakuwa nzuri. 

Nilicheza nao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa (2015, akiwa Juventus),” alisema Pogba. Kiungo huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na timu kubwa za Ulaya.

Mbali na hapo amepongeza muundo wa Barcelona na kueleza kuwa staa wa timu hiyo, Lionel Messi bado ni mchezaji mwenye kiwango cha juu. “Ni mchezaji bora wa muda wote, Barca ina wachezaji wengi wazuri,” alisema Pogba.

Comments