BEKI MPYA MBRAZIL WA SIMBA ALIVYOJICHANGANYA NA NEYMAR, COUTINHO NA KIPA WA LIVERPOOL

Simba imemshusha beki wa kati, Gerson Fraga Vieira raia wa Brazil na kuzua kubwa kubwa kuhusiana na usajili huyo.
Tayari wako wanaokosoa na wengine wanasifia hata kabla ya klabu ya Simba kutangaza rasmi kusajili kuhusiana na beki huyo aliyewahi kukipiga nchini India.
Kwa kuwa Brazil ni maarufu kwa soka, wengi wangependa kujua kuhusiana na Vieira ambaye kwa muonekano wa picha anaonekana ni beki hasa.
Beck huyo amezaliwa katika mjini mdogo wa Porto Alegre nchini Brazil. Umri wake sasa ni miaka 26 kwa kuwa alizaliwa Oktoba 4, 1992.
Ana uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya vichwa na pia ana uwezo wa kucheza nafasi kadhaa kama beki wa kati, beki wa pembeni na kiungo mkabaji.
Si mchezaji mdogo kwa kuwa alianza kujifunza soka katika klabu kubwa ya Gremio akianza mwaka 2000 hadi 2013.
Gremio Academy inajulikana kwa uzalishaji wa vipaji kwani hata nyota Ronaldinho alijifunza hapo soka kabla ya kuwa maarufu barato Ulaya na baadaye duniani kote.
Akiwa kinda alipata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya watoto chini ya miaja 15 na kuiongoza kubeba ubingwa wa Mediterranean International Cup.
Aliendelea kupanda hadi timu ya taifa ya Brazil chini ya miaja 17, wakati huo akiwa pamoja na nyota kama Neymar, Philippe Coutinho pia kipa namba moja wa Liverpool sasa Allison Becker.
REKODI ZAKE TIMU KUBWA
2013 - 2015.... Gremio ya ligi ya Brazil (Seriea A)
2016 - 2017.....Mumbai City ipo Indian Super League.
2017 - 2018.....Renota Yamagushi ya Japan.
Juni 30, 2018 - 31 May 2019 alijiunga na Mabingwa wa India Alletico de Kolkata ATK.
Baadaye alirejea Brazil ambako alijiunga tena na akademi ya Gremio ili kuendeleza vijana.


Comments
Post a Comment