TIBOROHA ATAKA WACHEZAJ WA KIGENI WAPUNGUZWE



Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Jonas Tiboroha ameungana na kauli ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe juu ya kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni nchini.

Katika siku ya Yanga Kubwa Kuliko iliyofanyika Jumamosi iliyopita, Mwakyembe alisema kuwa inabidi wachezaji wa kigeni wanaocheza ndani ya mechi wawe watano pekee ili kuwapa nafasi wazawa.

Waziri Mwakyembe aliamua kufunguka hilo akiwa na lengo la kuwapa nafasi zaidi wazawa kwa malengo ya kukijenga kikosi cha timu ya taifa ili ije kuwa na vipaji vizuri zaidi kwa siku za usoni.

Kutokana na kauli hiyo, Tiboroha ameiunga mkono akiamini itasaidia zaidi kukua kwa soka la Tanzania haswa kwa wachezaji wazawa ambao watakuwa tegemo ndani ya Taifa Stars.

Aidha, Tiboroha ambaye pia aligombea nafasi ya Uenyekiti Yanga katika uchaguzi mkuu ambao Mshindo Msolla aliibuka na ushindi, ameeleza kupewa nafasi kubwa kwa wazawa kutasaidia kuongeza vipaji kwa manufaa ya Stars.

"Naungana na kauli ya Mwakyembe juu ya kuweka idaidi ya wachezaji watano wa kigeni kucheza katika mechi moja.

"Hii itasaidia kuleta vipaji ambavyo vitakuwa na faida kwa timu yetu ya Taifa Stars haswa kwa siku za usoni." amesema.

Comments