Goli la Chama #hatariiiiiii
Clatous Chota Chama ‘Triple C’ alifunga goli ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba ili timu yao ifuzu hatua ya makundi ya ligi vilabu bingwa Afrika.
Baada ya goli hilo, shangwe kubwa iliripuka kutoka kila pembe ya uwanja wa taifa kusherekea goli hilo ambalo liliipa Simba ushindi wa magoli 3-1.
Mechi iliyochezwa Zambia Simba ilipoteza baada ya kufungwa 2-1 na Nkana FC, kwa hiyo Simba imefuzu hatua ya makundi kwa jumla ya magoli 4-3 na hii ni mara ya kwanza tangu miaka 15 iliyopita.
Comments
Post a Comment