Simba imefungwa magoli ya ajabu!!



Simba imeondolewa kwenye mashindano ya kombe la TFF (Azam Sports Federation Cup) baada ya kufungwa 3-2 na Mashujaa FC ya Kigoma.
Magoli yote matatu (3) ambayo Mashujaa wameifunga Simba ni kama ya maajabu kwa hususan goli la ushindi ambalo lilitokana na umakini mdogo wa golikipa wa Simba Dida kushindwa kuuzuia mpira.
Simba imeyaanga mashindano hayo katika raundi ya kwanza baada ya kushindwa kufuzu katika hatua ya 32 kama ilivyokuwa katika msimu uliopita ambapo ilitolewa kwa penati kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Green Warriors.

Comments

Popular Posts