AZAM FC YATUMA SALAMU KWA TIMU HII LIGI KUU
MABINGWA wa Afrika Mashariki na kati, Azam FC, wamewatumia salamu wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mchezo wao wa Ligi Kuu utakaochezwa jumamosi uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.
Azam FC wanashika nafasi ya pili kwenye Ligi wakiwa na pointi 40 baada ya kucheza michezo 16 wakiwa bado hawajapoteza mpaka sasa mchezo wowote.
Ofisa habari wa Azam, Jaffary Maganga amesema ugumu uliopo kwenye ligi unawafanya wazidi kupambana kujiaandaa vema zaidi hasa kutokana na ubora wa wapinzani wao Mtibwa kwa sasa.
"Sio timu ya kubeza ukizingatia kwamba wametoka kushiriki michuano ya kimataifa wana ule utofaui, ila kikubwa benchi la ufundi likiwa chini ya Hans Pluijm limefanikiwa kufanya kazi kubwa ya kuandaa kikosi na lengo ni kuendleleza rekodi yetu," alisema.
Comments
Post a Comment