BAAADA YA KUPIGWA NA MASHUJAA , HESABU ZA MBELGIJI ZIPO HIVI



KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa ana kazi kubwa ya kuweza kupata matokeo mbele ya kikosi cha Singida United katika mchezo wa Ligi kuu utakaochezwa jumamosi uwanja wa Taifa.

Simba wana pointi 30 wakiwa nafasi ya 13 baada ya kushinda michezo 9 na kupata sare 3 huku wakiwa wamepoteza mchezo 1 kwenye mzunguko wa kwanza.

Aussems amesema kuwa duniani hakuna kocha ambaye anaingia uwanjani akiwa na hesabu za kupoteza mchezo wake hivyo naye ana imani ya kupata ushindi.

"Malengo makubwa na kitu ambacho huwa nawaelekeza wachezaji ni kutafuta pointi tatu uwanjani hali itakayotufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye ligi.

"Wachezaji wangu wanauwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo uwanjani hali inayowafanya niwaamini ila tatizo lao ambalo huwa nalifanyia kazi ni safu ya ushambuliaji kukosa umakini wakiwa eneo la hatari, ila tutapambana," alisema.

Comments

Popular Posts