Boban atuliza presha Yanga



Taarifa kutoka Yanga zinasema mchezaji wao mpya Haruna Moshi ‘Boban’ atakuwepo katika orodha ya wachezaji watakaosafiri kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi guu dhidi ya Mbeya City.
Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amezungumzia kuhusu maendeleo ya afya ya Boban ambaye alipata maumivu katika mchezo wa kombe la TFF dhidi ya Tukuyu Stars ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo.
“Ilikuwa ni ‘soft injury’ alipata mshtuko kidogo kwenye nyonga lakini anaendelea vizuri amefanya mazoezi mepesi ya kukimbia mchangani (jana) na leo atakuwepo mazoezi ya asubuhi”-Dismas Ten, afisa habari Yanga.
“Nimezungumza na daktari, ameniambia kwamba anaendelea vizuri na hakuna mashaka juu yake ilkuwa ni mshtuko kidogo kwa sababu ya mechi tuliyocheza ilikuwa na nguvu mwanzoni lakini mwisho wa siku yupo vizuri na ataendelea na matibabu kama daktari ataona afya yake haijaimarika vizuri.”
Watu wengi walianza kudhani Boban huenda ana bahati mbaya baada ya kuumia katika mchezo wake wa kwanza Yanga na wapo waliofikiri labda angekaa nje kwa muda mrefu lakini yuko poa kama Dismas alivyoeleza.

Comments

Popular Posts