hiyo thamani ya bao la mkude ni shida, kotei afunguka



Simba jana ilifanikiwa kutinga kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushinda kwa mabao 3-1 Nkana FC ya Zambia kwenye mchezo wa marudio na kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 4-3.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Taifa, Nkana walikuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza dakika ya 16 kupitia Walter Bwalya aliyefunga kwa kichwa akitumia pasi ya Harrison Chisala, dakika ya 29, Jonas Mkunde alisawazisha kwa shuti kali akiwa nje ya 18 akimalizia pasi ya Claytous Chama.

Kiungo mkabaji wa Simba, James Kotei ambaye alifanikiwa kutoa pasi ya bao la pili dakika ya 45 lililofungwa na Meddie Kagere amesema thamani ya bao la Mkude ni kubwa kama ilivyo gharama za ndege aina ya Airbus.

"Ni bao zuri na lilikuwa ni muhimu kwetu kuweza kupata nguvu ya kupambana kwa ajili ya timu yetu, kwa furaha kubwa tuliyonayo unaweza kusema ni kama thamani ya ndege ya Airbus.

"Hakuwa katika mazingira ya kawaida ambayo yangemruhusu kufunga bao na alifanya maamuzi ambayo yaliwashangaza wengi hivyo thamani ya bao lake ni kubwa," alisema Kotei.
Bao la ushindi lilifungwa na Claytous Chama dakika ya 88 kwa staili ya kisigino akimalizia pasi aliyopewa na kiungo mwenzake Hassani Dilunga.


Comments

Popular Posts