KILUVYA UNITED YAFICHUA KILICHOWAPONZA KWA MTIBWA SUGAR
BAADA ya kikosi cha Kiluvya United kupoteza mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kichapo cha mabao 3-0, uongozi wa Kiluvya United umefichua kilichowaponza.
Ofisa habari wa Kiluvya United, Steven Kinabo ambayo kwa sasa inatumia jina la Rufiji United amesema kuwa kilichowaponza ni umakini wa wachezaji pamoja na kutokuwa na uzoefu kwenye mashindano makubwa.
"Kikosi kipo sawa na maandalizi yalikuwa sawa ila kikubwa ambacho kimetushinda ni uzoefu, wachezaji wetu wengi hawajashiriki michuano hii mara nyingi, ila ni sehemu ya kujifunza na kukomaa zaidi," alisema.
Jana timu mbili ziliaga mashindano na kuweka rekodi ya usawa ambapo moja ni ile inayoshiriki Ligi Kuu Simba kwa kutolewa na Mashujaa timu inayoshiriki Daraja la kwanza huku Kiluvya inayoshiriki daraja la kwanza ikitolewa na Mtibwa inayoshiriki Ligi Kuu.
Comments
Post a Comment