MASHUJAA" SIMBA WAMECHEZA MPIRA SISI TUMEONDOKA NA USHINDI



 KOCHA wa Mashujaa, Atugo Manyudo amesema kikosi cha Simba kilicheza mpira kwa kujituma ila wao wakatumia makosa yao kuweza kupata matokeo ambayo walikuwa wanahitaji katika mchezo huo.

Mashujaa ya Kigoma ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ilifanikiwa kuitoa kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho kwa kuifunga mabao 3-2 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jana.

"Nilitambua kwamba Simba wanacheza mchezo wa pasi nyingi na ni wazuri kwenye kushambulia hivyo tuliwabana wasicheze kwa uhuru na tukafanikiwa katika hilo kupata matokeo ni jambo jema.

"Walituzidi mbinu kipindi cha kwanza wakapata bao la kwanza ila kipindi cha pili nilibadili mbinu na kuwafanya wachezaji wacheze kwa umakini, hivyo wao wamecheza mpira sisi tumepata matokeo," alisema.

Simba inaweka rekodi ya kipekee kwa kutolewa mara mbili katika michuano ya FA na timu za Daraja la kwanza kwa kuwa hata msimu uliopita walitolewa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati na leo wakitolewa ndani ya dakika 90.

Comments

Popular Posts