MTIBWA SUGAR WAAHIDI KUIFANYA KITU MBAYA AZAM



KOCHA mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa amewapa mbinu kali wachezaji wake ili kuweza kufanikiwa kutibua rekodi ya Azam FC ya kutofungwa mpaka sasa katika michezo waliyocheza Ligi Kuu.

Mtibwa wataavaana na Azam FC jumamosi katika uwanja wa Manungu uliopo Morogoro ukiwa ni mchezo wa kiporo kwa Mtibwa kutokana na kushiriki michuano ya kimataifa.

Katwila amesema upinzani uliopo kwenye Ligi unamfanya awe makini asiweze kupoteza mchezo wake dhidi ya Azam na anatambua kwamba bado hawajafungwa hivyo atakabiliana nao kwa namna ya kipekee.

"Nawatambua wapinzani wetu hawajafungwa mpaka sasa hivyo nimewaambia wachezaji kwamba wanapambana na timu ngumu ambayo haijafungwa mpaka sasa ila wao wana uwezo wa kuwafunga na kuandika rekodi mpya," alisema

Comments

Popular Posts