Mwl. Kashasha kawachana Simba



Mchambuzi wa soka Mwl. Alex Kashasha katika uchambuzi wake wa mchezo wa mechi ya Simba vs Mashujaa (Azam Sports Federation Cup) amesema dharau ya Simba na kuwachulia poa wapinzani wao ndio kitu kilichowaponza na kujikuta wakipoteza mechi na kutolewa kwenye mashindano hayo.
“Kwenye mashindano haya kila timu inatakiwa iamini kwamba kila anaekuja kucheza anakuja kushindana, sasa unapoona unacheza na timu ya kiwango cha chini kama Mashujaa maana yake unawasaidia waoneshe walichonacho”-Mwl. Kashasha.
“Kwa hiyo wakati mwingine wapinzani inabidi kuheshimiana haijalishi upo ligi kuu au daraja la kwanza ilimradi mnacheza shindano moja.”
“Kichuya alipata mipira mingi akiwa free lakini attempt zake zote zilikuwa off target inawezekana hesabu zake hazikuwa vizuri au alikuwa anakosa timing lakini pia.”

Comments

Popular Posts