obrey chirwa adaiwa makombe haya azam fc
Uongozi wa Azam FC, umesema kuwa baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji wao Obrey Chirwa ana kazi kubwa kuhakikisha anaipatia makombe matatu ambayo atashiriki.
Azam FC wanashiriki kwenye mashindano matatu ambayo ni Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na wakiwa ni watetezi wa kombe la Mapinduzi litakalofanyika Zanzibar Desemba 30.
Ofisa habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema wamekamilisha taratibu zote za mchezaji Chirwa ambaye amesajiliwa kwa kandarasi ya mwaka mmoja akiwa ni mchezaji huru ambaye alikuwa akiitumikia Nogoom ya Misri.
"Kazi kubwa tumekamilisha kwa mchezaji wetu ambaye anaanza kazi yake ndani ya Azam FC, kikubwa anachotakiwa kufanya akiwa na wachezaji wenzake ni kuisaidia timu iweze kubeba makombe katika mashindano tunayoshiriki.
"Tunashiriki Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho pamoja na kombe la Mapinduzi ambalo sisi ni mabingwa watetezi, tunachohitaji ni kubeba makombe yote na hili la Mapinduzi tunalitaka jumlajumla kwa kuwa tumelibeba mara mbili mfululizo," alisema.
Comments
Post a Comment