Prisons yafunguka kocha kutimuliwa
Baada ya taarifa kusambaa kwamba Tanzania Prisons imemsitishia mkataba kocha wake mkuu Abdallah Mohamed, Katibu wa klabu hiyo Havinitishi Abdallah amekanuha taarifa hizo.
“Hizo habari si za kweli kabisa mwalimu wetu Bares bado tunae, hakuna habari yoyote kwamba ameondoka. Tutafatilia nani amezieneza hizo taarifa tutamchukulia hatua kwa sababu amesema kitu ambacho hakipo.”
Kocha wa Tanzania Prisons Abdallah Mohamed ‘Bares’ amesema bado anaendelea kuwa kocha wa timu hiyo licha ya taarifa kusambaa kwamba amesitishiwa mkataba wake na ‘Wajelajela’.
“Taarifa hizo si za kweli bado nipo Tanzania Prisons, hizo ni taarifa ambazo hata mimi nazisikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Bado nipo na uongozi wangu lakini wenye watakapoamua au nitakapoamua mwenyewe tutatangaza, kwa sasa bado suala hilo halipo.”
“Hizi tetesi hazinitishi, bado naithamini kazi yangu kama niliingia basi ipo siku nitatoka japo sijui ni kwa njia gani kama ni kuondoka mwenyewe au kusimamishiwa mkataba wangu.”
“Bado nipo na tunashirikiana vizuri na uongozi wa Tanzania Prisons, hizo ni habari ambazo zinasemwa kwa wingi kwa hivi sasa.”
Comments
Post a Comment