TAMBWE APANIA MAKUBWA MBEYA



MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amissi Tambwe amesema  kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuikabili Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa jumamosi uwanja wa Sokoine.

Tambwe ana rekodi ya kufikisha jumla ya 'hattrick' 7 kwenye ardhi ya Bongo na zote katika uwanja wa Taifa, 2013/14 akiwa Simba alifikisha 3, 2015/16 alifikisha 3 akiwa Yanga zote ikiwa ni Ligi kuu na 1 ya hivi karibuni akiwa Yanga ikiwa ni ya kombe la Shirikisho.

Tambwe amesema hatua hiyo aliyofikia kwa sasa ni salamu kwa wapinzani wake Mbeya City ambao watacheza nao mchezo wa Ligi Kuu Desemba 29.

"Muda mrefu nilisubiri kuweka rekodi mpya na haikuwa rahisi kufanikiwa kutokana na ushindani, ila nimefanikiwa ni jambo la kushukuru na kuongeza zaidi juhudi kuisaidia timu yangu mpaka kupata matokeo.

"Tuna kazi kubwa mbele yetu Ligi kuu na upinzani ni mkubwa ila nina imani tutafanya vizuri hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti bila kuchoka," alisema Tambwe.

Tambwe amehusika kwenye mabao 5 kati ya 33 waliyoyafunga kwa sasa wakiwa ni vinara wa Ligi baada ya kucheza michezo 17 na pointi 47 kibindoni.

Comments

Popular Posts