ZAWADI NONO MAPINDUZI CUP ZAWEKWA HADHARANI



Mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2019 yataanza kutimua vumbi lake tarehe 1 Januari na kumaliza tarehe 13 Januari 2019, yakihusisha timu 9 badala ya 10 kama ilivyotangazwa awali.

Timu 6 zitakazoshiriki kutoka Zanzibar ni KVZ, KMKM, Jamhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi huku timu 3 za Azam, Simba na Yanga zikitoka Tanzania Bara.

 Timu hizo zimepangwa katika makundi mawili ambapo Kundi A linajumisha timu za Chipukizi, Mlandege, KMKM na Simba wakati Kundi B litakuwa na timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga. Mechi zote katika mashindano hayo zitakufikia mbashara kupitia Azam TV.

ZAWADI

Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo imesema kuwa zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka shilingi milioni 10 hadi kufikia shilingi milioni 15 ikiwa ni pamoja na medali za dhahabu pamoja na kombe.

Mshindi wa pili naye naye atapata shilingi milioni 10 badala ya milion 5 iliyokuwa ikitolewa awali, na medali za fedha.

Kama Azam FC watachukua kombe hili mwaka huu wa 2019, Kombe litakuwa ni mali yao kwa mujibu wa kanuni kwani watakuwa wamelichukua kwa miaka 3 mfululizo”, amesema Said.

TIMU KUTOKA NJE YA TANZANIA

Kuhusu kukosekana kwa timu kutoka nje ya Tanzania, Said amesema timu ya URA ambao walijiandaa kushiriki mashindano haya na kuthibitisha ushiriki wao wameshindwa kupata kibali kutoka Chama cha Mpira wa Miguu cha Uganda (FUFA) kutokana na kubanwa na ligi kuu nchini kwao.

Amesema walipeleka pia mualiko nchini Kenya lakini nao walijibu kuwa wametingwa na ligi kuu kwa hiyo wasingeweza kuiruhusu timu ya Bandari ambayo ilikuwa tayari kushiriki mashindano hayo.

VIWANJA

Mashidano hayo msimu huu yatafanywa katika viwanja vya Amaan (kwa mechi zote mpaka nusu fainali) na Uwanja wa Gombani kwa mechi ya fainali.

Mechi za Amaan zitakuwa zinachezwa saa 10:15 jioni na saa 2:15 usiku huku mechi ya fainali ikitarajiwa kuchezwa saa 9:30 jioni.

Comments

Popular Posts