Abdi Kassim alisajiliwa kwa 3.5M na mshahara wa 150,000 kwa mwezi



Star wa zamani wa Mtibwa Sugar, Yanga pamoja na timu ya taifa Abdi Kassim ‘Ballack wa Unguja’ amesema wakati anasajiliwa na Mtibwa Sugar kutoka Mlandege dau lake lilikuwa ni shilingi milioni 3.5.
Alianza kwa kulipwa mshahara wa shilingi 150,000 (laki moja na elfu hamsini) kwa mwezi, alichagua kwenda Mtibwa licha ya kutakiwa na vilabu vya Simba na Yanga lakini alishauriwa aanzie Mtibwa ili apate uzoefu kwenye ligi ya Tanzania bara.
Abdi amesema wakati huo alikuwa mdogo kiumri hivyo kutoka moja kwa moja Mlandege kwenda Simba au Yanga huenda kungeua kipaji chake.
Baadaye akasajiliwa Yanga na baadaye Malaysia ambako aliongeza kipato chake.

Comments

Popular Posts