ALIYEIPA DOZI TATU PEKEE YANGA AIKANA LIGI YA BONGO


ALIYEKUWA mshambuliaji wa Stand United ambaye alifanikiwa kuifunga Yanga mabao matatu 'hat trick' Alex Kitenge amesema kwa sasa hana mpango wa kurejea Bongo kutokana na mipango kumyookea nchini China.

Kitenge ambaye tangu aifunge Yanga amebaki na mabao matatu mpaka sasa licha ya kucheza mechi nyingine hatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi Uwanja wa Karume mkoani Shinyanga.

Kitenge amesema kwa sasa hafikirii kurejea nchini Tanzania kuendelea kuitumikia klabu yake ya Stand United kutokana na kutolipwa stahiki zake kwa muda mrefu pamoja na kupata timu mpya China.

"Sipo Bongo muda mrefu natafuta maisha mapya huku China na ninashukuru kila kitu kinakwenda sawa nimeanza kazi baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwenye timu yangu mpya ya Macao Club ninayoitumikia huku China.

"Nitawakosa rafiki zangu Yanga ila ninaamini wachezaji wenzangu watafanya vizuri kwa kuwa wana uwezo mkubwa wa kupambana na kupata matokeo nafasi wanayo wanapaswa watulie wasiwe na presha kila kitu kitakuwa sawa," alisema Kitenge.

Comments

Popular Posts