“Kagere kuanzia benchi haikuwa bahati mbaya”
eddie Kagere alianzia benchi vs Saoura, kwa siku za hivi karibuni kocha wa Simba Patrick Aussems amekuwa akiwaanzisha washambuliaji watatu kwa pamoja (Okwi, Bocco na Kagere) lakini jana ilikuwa tofauti.
Inawezekana watu wengi walidhani Kagere kuanzia benchi ilikuwa ni kutokana na majeraha madogo aliyopata kwenye #MapinduziCup, lakini kwa upande wangu naamini ilikuwa ni mbinu za kocha hivyo haikuwa bahati mbaya kuanzia benchi.
Unapocheza na timu kutoka Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika inabidi ufahamu nguvu yao kubwa ipo eneo la katikati ya uwanja (midfield) kwa hiyo alichofanya Aussems ni kupunguza mshambuliaji mmoja ili apate nafasi ya kuongeza viungo ndiyo maana Simba ilianza na viungo wanne (Kotei, Mkude, Chama, Dilunga) kwa pamoja.
Simba ilifanikiwa katika eneo la midfield na kutawala mchezo, hata walipopoteza mpira waliupata kwa haraka na kuurudisha kwenye himaya yao.
Bocco alipoumia na kushindwa kuendelea na mchezo Kagere akapewa nafasi, kumbuka alikuwa benchi anausoma mchezo na kubaini ubora na udhaifu wa walinzi wa Saoura.
Kagere ni mchezaji anayetumia vizuri mbio pamoja na nguvu. Anakuwa kwenye nafasi mwafaka katika wakati mwafa, pia anajua kutumia nafasi kwa ufasaha. Washambuliaji wengi wana sifa mbili za kwanza (kuwepo kwenye nafasi mwafaka katika wakati mwafaka) sifa ya tatu wengi wao wanaikosa lakini Kagere hahitaji nafasi zaidi ya 3 kufunga goli 1.
Kwa uwezo aliouonesha jana, licha ya kuanzia nje lakini alifanikiwa kufunga magoli mawili. Nampa 8/10 katika mchezo wa jana, Kagere alifanikiwa lakini pia kocha alifanikiwa.
Comments
Post a Comment