KOCHA ALIEWAHI KUINOA SIMBA AANZA KWA KUAIBISHWA SINGIDA
KOCHA mpya wa Singida United, Mserbia Dragan Popadic kwa kushirikiana na Dusan Momcilovic ambaye ni Kocha Msaidizi ambao waliwahi kuifundisha Simba, wameanza kwa kupokea kichapo katika mchezo wao wa kwanza wakiwa Singida United.
Kocha huyo ambaye kazi yake kubwa ni kufanya mabadiliko ya kikosi ili kipate matokeo chanya ana kandarasi ya miezi sita ndani ya kikosi hicho akichukua nafasi ya Hemed Morroco.
Mchezo wake wa kwanza jana alipoteza dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Raphael Siame dakika ya 72 akimalizia pasi ya Pastory Athanas.
Ofisa Habari wa Singida, Cales Katemana amesema kuwa walipambana kutafuta matokeo ila wamepoteza wanajipanga kwa ajili ya mchezo wao unaofuata.
Comments
Post a Comment