Simba inaendekea kurundika viporo ligi kuu
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amethibitisha kusogezwa mbele mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Lipuli FC dhidi ya Simba uliokuwa uchezwe kesho kwenye uwanja wa Samora-Iringa.
Simba sasa inatofauti ya michezo 7 na timu nyingine ambazo zimeshacheza mechi 21 wakati Simba imecheza mechi 14.
“Mchezo wa Simba na Lipuli tumeshauondoa, ndani ya siku mbili tutatangaza ratiba ambayo itajumuisha mechi zote za viporo mashindano ya SportPesa kwa kuzingatia ratiba ya mechi za Azam Federation Cup.”
“Ligi inaendelea ushindani umekua mkubwa, changamoto ya viporo tunajua sababu zinazosababisha inakuwa hivyo na hii si kwetu peke yetu inatokea hata kwenye ligi nyingine kwa sababu kuna timu zinakuwa na majukumu mengine.”
“Mwisho wa siku ligi itachezwa na kuisha huku timu zote zikiwa na idadi sawa ya mechi.”
Comments
Post a Comment