Simba yamchinjilia mbali mwarabu taifa, yapata ushindi mnono mbele ya Waziri Mkuu, Okwi, Kagere moto
Klabu ya Simba sport club kutoka jijini Dar Es Salaam, mitaa ya Kariakoo imefanikiwa kuigaragaza klabu ya JS Saoura kutoka nchini Algeria katika dimba la Taifa jijini Dar Es Salaam.
Ikicheza kandanda la aina yake mbele ya Waziri Mkuu Mh. Kassimu Majaliwa, klabu hiyo imefanikiwa kupata ushindi mnono katika kundi lake la D. Mesie Kagere akifunga goli mbili goli la pili na la tatu huku goli la kwanza likikwamishwa kimiani na Emanuel Okwi
- Ikumbukwe kwamba JS Saoura anachezea Mtanzania Thomas Ulimwengu, hivyo Simba wanakuwa vinara katika kundi lao wakijikusanyia alama 3 na magoli 3, mbele ya Al ahly ya Misri, JS Saoura na AS Vita club kutoka nchini DR Congo.
Comments
Post a Comment