Wazungu na wadau wanasemaje kuhusu tetesi za Samatta
Baada ya vyombo vichache kueneza kuhusu sakata la Samatta kuhusishwa na klabu ya nchini Uingereza Cardiff. Nilipata bahati ya kuchunga mitandaoni hali ipo. Wapo ambao wanajiuliza huyu Samatta ni nani? Wengine wana wasiwasi na ligi anayotoka na wengine hawaamini kabisa kama Samatta ni chaguo sahihi.
Kila mtu ana mawazo yake katika hili.
Huyu anaona usajili wa Samatta au Niasse itakuwa moja ya njia nzuri za kuimarisha bajeti na soko. Yeye anaamini kuwa dau la Samatta ni zuri na kama atasajiliwa akashindwa kufit mfumo bado kutokana na umri wake Cardiff itaweza kumuuza kwa bei nzuri.
Huyu Kwasi ni raia wa Ghana. Yeye ina imani kuwa Samatta ni chaguo sahihi zaidi kwa Cardiff.
Lee Martin mzaliwa wa kule kule Cardiff anaishauri Cardiff kuwa waachane na Emiliano Sala kisha wamchukue Samatta kutokana bei ya Samatta kuwa ahueni na umri wake bado ni bingo kwa Cardiff.
Paul Gronow anasema watu wanaofuatilia ligi ya Ubelgiji wamemwambia Samatta ni mtu hatari sana. Hivyo ni injinia mzuri atakayeweza kuwasomesha mashabiki wake ipasavyo
Jeff Paker amemwagia sifa kedekede Samagoal kuwa ni mshambuliaji mwepesi ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani. Yeye anaamini kuwa Zohore ni mzuri kuliko Sala hivyo kuna uwezekano sana akala mkeka. Ni aibu kwa Mchezaji wa £20M kukaa benchi wka klabu ndogo kama Cardiff. Hivyo Samatta ni mchezaji sahihi kwani hategemei kucheza eneo moja tu (9) kama ilivyo kwa Sala na Zohore.
Lee Johnson hajui lolote kuhusu Samatta. Lakini amekuwa tu na imani na Samatta baada ya kusikia ni mmoja kati ya watu hatari sana huko kwa akina Lukaku. Ningekuwa na namba ya simu ya Lee ningemuuliza hivi hakusikia kama Samatta ana goli 9 kwenye mechi 10 za Yuropa? Yaani hajui kama Samatta ana magoli mengi kuliko wachezaji wa Arsenal na Chelsea huko Yuropa au kiburi tu?
Clam hataki maneno mengi amesema hao Sala na Zohore kwa Samatta watasubiri.
Comments
Post a Comment