ZAHERA AONGEZA MASHINE MBILI KALI YANGA KUWANYIMA SIMBA UBINGWA
Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu kumalizika kwa mashindano ya Mapinduzi CUP huko Zanzibar, Kocha Mkuu wa Yanga amewapandisha daraja wachezaji wawili waliokuwa sehemu ya kikosi visiwani humo.
Mwinyi Zahera ametangaza kuwapandisha mpaka kikosi A wachezaji Shaibu Ramadhan na Gustavo Simon baada ya kuonesha kiwango kizuri Mapinduzi.
Kocha huyo alieleza kuvutiwa na uwezo walioonesha kwenye michuano hiyo licha ya kuwa hakusafiri na timu na badala yake alikuwa akitazama mechi kupitia Azam TV.
Wakati huo kikosi cha Yanga leo kimesafiri kuelekea Shinyanga ambapo kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa CCM Kambarage Stadium.
Comments
Post a Comment