Azam yaduwazwa Mbeya



Tangu January 2019, Tanzania Prisons imepoteza mchezo mmoja tu (January 2, 2019-Lipuli 1-0 Tanzania Prisons) baada ya hapo wamecheza mechi 8 mfululizo bila kupoteza.


Wametoka sare katika mechi mbili na kushinda michezo mitano ya ligi kuu Tanzania bara.
Mechi 4 zilizopita za Tanzania Prisons Ligi kuu Tanzania bara 2018/19.
Kagera Sugar 0-2 Tanzania Prisons
Tanzania Prisons 2-1 Mbao
Tanzania Prisons 1-0 Stand United
Tanzania Prisons 1-0 Azam
Kipigo walichopata Azam leo toka kwa Tanzania Prisons ni cha pili kwao msimu huu baada ya kuchapwa na kwa mara ya kwanza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu, Turiani-Morogoro.
Azam haijashinda mechi tatu mfululizo zilizopita za ligi kuu Tanzania bara imetoka sare mbili na kupoteza mbele ya Prisons.
Azam 1-1 Alliance
Azam 1-1 Lipuli
Tanzania Prisons 1-0 Azam.

Comments

Popular Posts