Baada ya Simba kumpiga Al Ahly, kocha wa Yanga kaongea
Kufatia ushindi wa jana wa Simba (1-0) dhidi ya Al Ahly uwanja wa Taifa, kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema timu zote kwenye kundi hilo (Al Ahly, Simba, JS Saoura na AS Vita) zina nafasi ya kusonga mbele kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.
Zahera amesema AS Vita ikija hapa kucheza na Simba mechi itakuwa ofauti na mechi ambazo Simba imecheza dhidi ya timu za kiarabu. Amesema Tanzania kuna wakongo wengi ambao wanaishi hapa hivyo inawezekana AS Vita wakawa wanapata taarifa za kiufundi kuhusu Simba.
“Nadhani timu zote nne zina fasi ya kupita kwenda hatua inayofuata. Vita Club itakuja hapa ndhani watakuwa tofauti na timu ya waarabu zilizokuja kucheza hapa”-Zahera Mwinyi, kocha Yanga SC.
“Vita Club wana watu wengi ambao wanaijua inchi hii (Tanzania) na walikaa sana hapa, itakuwa tofauti sana na timu za wa arabu. Nadhani mmejionea tafauti ya hizo timu zote nne kwenye kundi lao na nafasi ya kila timu kusonga mbele.”
Zahera anatarajia kukutana na Simba February 16, 2019 kwenye mchezo wa ligi unawakutanisha watani wa jadi Yanga vs Simba.
Comments
Post a Comment