Simba ilistahili ushindi vs Al Ahly
Mchezo wa Simba vs Ahly ulifatiliwa karibu na wapenda soka wa bara zima la Afrika kutokana na ukubwa wa Al Ahly. Unapoitaja Ahly ni timu ambayo kila pembe ya Afrika inafahamika kwa upande wa soka.
Watu wanashangaa Al Ahly iliyocheza na Simba Misri imekuwa tofauti na ambayo imecheza uwanja wa taifa, sawa na Simba iliyocheza Misri na iliyocheza uwanja wa taifa inaonekana kuwa ni timu mbili tofauti.
Watu wanatakiwa kutambua hizi ni mechi mbili tofauti, kwamba ile mechi ya kwanza (Al Ahly 5-0 Simba) game plan ya Simba haikufanikiwa kama ambavyo mipango ya Ahly ilivyokuwa.
Ukiangalia mechi ya kwanza Ahly kwa ile spirit ya kuwa nyumbani, toka dakika ya kwanza waliwekeza kwenye kushambulia. Mpanga mkakati wa game ile ilikuwa ni kushambulia kwa mipango kwa kufika kwenye goli la mpinzani mara nyingi na kutengeneza nafasi za kutosha kufunga magoli.
Wakafanikiwa kufunga magoli matano ndani ya kipindi cha kwanza plan yao ikawa imefanikiwa kipindi cha pili wakatulia ili wasitumie nguvu nyingi kwa sababu walishaua mchezo.
Wamekuja huku ni game tofauti, Simba iliyofungwa magoli matano imejiuliza kwa nini ilipoteza kwa magili matano kwenye mechi mbili mfululizo ugenini. Wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wao ambao walijitokeza kwa wingi na kuwapa hamasa ya kutosha walikuwa na jambo la kufanya kwa ajili ya mashabiki.
Ukiangalia plan ya kocha wa Simba Patrick Aussems aliingia kwa kuwaheshimu Al Ahly, alianza kuijenga timu kuanzia nyuma.
Safu ya ulinzi ya Simba iliyoanza ilikuwa na wachezaji wa ulinzi asilia, Zana ni baki kabisa alikuwa anakaba vizuri tofauti na Gyan ambaye muda mwingi hushambukia kwa kutanua uwanja na kuongeza idadi kwenye eneo la ushambuliaji kwa mpinzani. Wawa, na Juuko wachezaji wazoefu halafu Kwasi ambaye baadaye alimpisha Tshabalala.
Juu yao walikuwepo Kotei na Mkude, seti ya kwanza ya idara ya ukinzi ikawa imekamilika. Seti ya pili ilikuwa ni mbele kwenye eneo la ushambuliaji ambapo kwa bahati nzuri katikati yao yupo Chama ambaye ni mchezaji huru anakuwa anachezesha timu.
Okwi muda mwingi alicheza upande wa kulia na kufanya nyendo nyingi za Zana kuishia katikati halafu anarudi kwenye eneo la ulinzi. Meddie Kagere anakimbia na Bocco pia anauwezo wa kukimbia timu ikawa imebalance.
Plan waliyokujanayo Al Ahly ilikuwa tofauti na walivyokuwa nyumbani, huku walikuwa ugenini na wao walikuwa wanacheza kwa kuvizia iliwapate nafasi ya kushambulia kwa kushtukiza.
Ahly walikuwa wanajilinda zaidi, kama ulifatilia kipindi cha kwanza kila wachezaji wa Simba walipoingia kwenye box lao mara zote Ahly walikuwa wengi kwenye eneo hilo kuliko wachwzaji wa Simba maana yake ni kwamba muda mwingi wa mchezo Ahly walikuwa wanacheza kwenye eneo lao la kujilinda.
Kwa hiyo kwa timu nyingine ambayo inatakiwa ipate advantage kwa sababu wapinzani wapo kwenye eneo lao la kujilinda ilikuwa ni Simba ndio maana walipata kona nyingi (tisa dhidi ya moja) kona hizo zinatokea kwa sababu Simba walikuwa wanashambulia sana.
Simba ilipiga jumla ya mashuti 15 ambapo mashuti 5 yakilenga golo wakati Al Ahly walipiga jumla ya mashuti 5 huku shuti moja tu ndio likilenga lango, kwa takwimu hizi Simba walistahili ushindi.
Comments
Post a Comment