“Wao ndo wenye presha, sio sisi”-Zahera Mwiyi
Kuelekea mechi ya watani wa jadi Yanga vs Simba Jumamosi ijayo February 16, 2019, kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema timu yake inaendelea na mazoezi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo.
Zahera anasema wanajiandaa na mechi hiyo kama ilivyo kwa mechi nyingine na wao hawana presha ila presha ipo kwa Simba.
“Tuko vizuri maandalizi yameendelea vizuri, wachezaji wote 28 wamefanya mazoezi vizuri morali ya wa chezaji ni nzuri tokea tulirudi Tanga. Isipokuwa Kamusoko ndio alikua na matatizo kidogo ya nyama za mguu.”
“Jana tulifanya mazoezi na leo tuliendelea na kazi ya technical, tactical na jinsi ya kushambulia, kesho tunaendelea na kazi ya jinsi ya kujilinda.”
“Mechi ya Simba jana, unajuwa mpira siyo sawa na hesabu ya kusema 1+1=2, mpira sio kwa sababu ulimfunga X, basi utamfunga Y, hapana Jumapili sio Jumatatu.”
“Kama majina ya siku yako tofauti na timu za mpira duniani kote zipo tofauti. Al Ahly sio Yanga na Yanga sio Al Ahly.”
“Mechi ya Simba tunajitayarisha kama mechi ya Coasta Union, JKT Tanzania, Singida United na wengine woote. Ofauti na mechi nyingine tumekaa kambini siku mbili halafu mechi ya Simba tunakaa kambini kwa siku tano.”
“Kwa sababu mechi ya Simba imetukuta tumetokea kucheza Tanga, Singida, halafu Tanga tena kwa hiyo tuliona ni vizuri tuende kambini moja kwa moja tupate uwanja wa mazoezi muzuri Morogoro.”
“Mechi dhidi ya Simba ni mechi kama nyingine yoyote, tunacheza na Simba ambao walisema tangu mwanzo wa kwamba wao watabeba ubingwa lakini sisi Yanga mlisikia mwanzo wa ligi tunasema sisi tunacheza ligi mwaka huu ili kubeba ubingwa?
“Sasa kwa sababu gani mechi hii tuwe na presha? Sisi hatuna presha yoyote, ni wao ndio wana presha. Sisi tukishinda ni furaha, tukitoka sare ni furaha tukifungwa haibadirishi chochote kwenye malengo yetu ya mwaka huu.”
Comments
Post a Comment