BALE ATUA MAN UNITED



WINGA wa Real Madrid, Gareth Bale, wiki hii alikuwa na muda mzuri wa kufurahia kufanya mazoezi ndani ya viwanja ambavyo vinamilikiwa na Klabu ya Manchester United.

Bale ambaye aliwahi kuwaniwa na Man United, alifika kwenye uwanja wa mazoezi wa Man United, Jumanne ya wiki hii ambapo ndipo timu yake ya taifa inapotumia kufanya mazoezi, alikuwa gumzo kutokana na kuwahi kuhusishwa kwake na klabu hiyo.

Hata wakati akipita kwenye njia za kuingia ndani ya viwanja vya Aon Complex vilivyopo Carrington, alipigwa picha nyingi, hasa alipokuwa akipita katika ukuta uliokuwa na picha kubwa za wachezaji wa United.

Bale, 29, alitarajiwa kuongoza timu yake ya taifa juzi usiku kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Trinidad and Tobago lakini alipewa mapumziko na kocha wake, timu hiyo itacheza dhidi ya Slovakia, keshokutwa Jumapili.

Wales inatumia viwanja hivyo kwa mazoezi pamoja na kufikia katika Hotel Football ambayo inamilikiwa na kocha wa Wales, Ryan Giggs na patna wake, Gary Naville jijini Manchester.

Comments

Popular Posts