FIFA imetangaza mwezi itakao toa jibu la timu 48 za World Cup 2022 Qatar
Kuna uwezekano mkubwa fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika nchini Qatar zitashirikisha jumla ya timu 48 kutoka 32 zilizokuwa zinashiriki katika fainali zilizopita, hiyo ni baada ya uongozi wa juu wa soka FIFA kukaa kikao hivi karibuni na kujadili dhamira yao ya kuongeza timu.
Bado FIFA haijatoka uamuzi kamili kuhusu ongezeko la timu 16 za michuano hiyo katika list ya 32 zilizokuwa zinashiriki awali, uamuzi wa mwisho unatajwa kuwa utafanyika mwezi June mwaka huu 2019 lakini inaonekana viongozi wa juu wa soka wamedhamiria kutaka kuona hilo likitimia katika fainali za 2022.
Inaelezwa kuwa kama FIFA itaongezwa timu hizo na kuwa 48 katika fainali za Kombe la Dunia 2022 basi watatafuta nchi mwenyeji mwenza na Qatar wa michuano hiyo, huku nchi za Kuwait na Oman zikipewa kipaumbele kuwa zinaweza zikawa mwenyeji mwenza wa Qatar kama wazo la timu 48 za Kombe la Dunia 2022 litaanza kutumika 2022.
Comments
Post a Comment